Monday, April 16, 2012

THE 2012 EASTER CONFERENCE


 

Baadhi ya wana CASFETA-TAYOMI wakiwa wanamwabudu Mungu wakati wa kambi la Pasaka lililofanyika Arusha Mjini Katika Kituo Cha International Evangelism Centre- Sakila, Kambi hii ni moja ya makambi matatu yaliyofanyika mkoani Arusha, wana CASFETA zaidi ya 1500 walihudhuria. Habari kuhusu makambi mengine nchi nzima zitakufikia kupitia Blog hii hii.


TANGA

 Baadhi ya wana CASFETA-TAYOMI waliohudhuria kongamano la Pasaka wakisikiliza mafundisho ya neno la Mungu. Kongamano hili lilifanyika wilayani Lushoto katika chuo cha maendeleo ya jamii Mabugai Tarehe 5-9/4/2012. Watu zaidi ya 200 walihudhuria.


MAOMBEZI
Mchungaji Shetuli wa Evangelistic Assemblies of God (E.A.G.T) wilayani Lushoto akifanya maombezi kwa baadhi ya wana CASFETA wakati wa Kongamano la Pasaka la mwaka 2012 Mkoani Tanga.

VIPAJI

Vijana wenye vipaji waliigiza juu ya Kuteswa, kufa na kufufuka kwa YESU KRISTO kwenye Kongamano la Pasaka (2012) Mkoani Tanga, huyu kijana mwenye nguo nyeupe (Yesu) alionyesha kipaji cha ajabu kwa kusema maneno yote ya kwenye filamu ya Yesu bila kukosea, ilikua furaha ya ajabu.